Isaiah 66:10-12


10 a“Shangilieni pamoja na Yerusalemu na mfurahi kwa ajili yake,
ninyi nyote mnaompenda,
shangilieni kwa nguvu pamoja naye,
ninyi nyote mnaoomboleza juu yake.

11 bKwa kuwa mtanyonya na kutosheka
katika faraja ya matiti yake;
mtakunywa sana,
na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.”

12 cKwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: “Nitamwongezea amani kama mto,
nao utajiri wa mataifa kama kijito kifurikacho;
utanyonya na kuchukuliwa mikononi mwake
na kubembelezwa magotini pake.
Copyright information for SwhKC